The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Latest Posts

Tuesday, September 27, 2016

Papaa On Tuesday.....Tabia Yako Yaweza Kuwa Fursa ama Kikwazo

Papaa On Tuesday....Ukijua Tabia Yako Inakusaidia Kujua kama ni Fursa ama Kikwazo Cha Mafanikio Yako.

Hakuna mtu asiye na shauku ya kufanikiwa awe mzungu au muafrika ama muhindi awe mzima ama mlemavu, awe mwanamke ama mwanaume,mrefu ama mfupi kila mmoja anayo kiu ama shauku ya mafanikio.

Vipo vikwazo vya mara kwa mara ambavyo vimesababisha either mtu kufanikiwa ama kushindwa kufanikiwa. Moja ya sababu ya mtu kufanikiwa ama kutofanikiwa ni tabia. Iwe tabia ya kurithi ama tabia isiwe ya kurithi. Tabia yako inaweza kuwa sababu kubwa sana ya kuwa hapo ulipo. Zipo tabia nyingi sana ambazo zinaweza kukusaidia kupiga hatua za haraka ama za polepole katika mafanikio.

Tabia ya Umakini. Tafiti zinaonesha watu wengi waliofanya kwa kukurupuka walijikuta katika lindi la mawazo katika maamuzi. Wengi waliofanya maamuzi pasipo umakini walijikuta wakipata hasara,wakipoteza muda,wakitapeliwa sababu waliwahi sikia ukifanya ukifanya jambo filani utatoka kimaisha mwisho wa siku walijikuta wamefanya pasipo umakini wakajikuta katika majuto.

Tabia ya Kutapanya Fedha. Kuna msemo unasema pata fedha tujue tabia yako. Fedha ina kanuni zake katika maisha. Tabia ya kukosa nidhamu ya fedha imekwamisha wengi. Unakuta ukiwa na fedha unaishia kununua simu,nguo,magari,chips na mayai. Siku ukiwa huna hela ndo unakumbuka biashara, mashamba, hisa basi tambua kuwa nidhamu ama utapanyaji wa fedha unakuvusha ama inakukwamisha.

Uwezo wa Kupata Taarifa za Fursa na Kuamua kwa Wakati. Mafanikio sio miujiza ni uwezo wa kupata taarifa na kuamua. Watu wanakuzunguka wanazotaarifa za kutosha kuhusu unakotaka kwenda. Una ndoto ya kufanyakazi UN,Una ndoto za Kujiajiri, Unandoto za Kuwa Msomi unadhani mazingira uliyonayo yanakupa taarifa za Kutosha kuhusu ndoto zako?Unapata wapi taarifa zinazoweza kuku challenge maamuzi yako. Ukitaka kupanda ndege hata kama tiketi unayo first class ndege haikufati nyumbani. Hakuna jambo halina Kanuni wala Mchakato. Unazo taarifa sahihi ngapi za mikopo?una taarifa ngapi sahihi kuhusu Kilimo wengi wetu tuna taarifa za tetesi kisha tunafanya maamuzi. Wengi waliofanikiwa ni kwamba waliziona fursa ama walizisikia na wakaamua kufanya maamuzi haraka.

Kughaili Ghaili kufanya Maamuzi. Mwaka jana ulisema mwaka huu saa hizi tayari umeshasema mwakani kumbuka mwaka uleee ulisema hivyo hivyo. Kila siku unasema kuna mambo unakamilisha halafu unaamua kikweliii kweliii. Tabia ya kughaili kufanya maamuzi imekusababishia kuishia kufanya tu mipango lakini haitekelezeki. Familia haisogei sababu kila mwaka unasema mwakani, unasema kesho. Miaka itapita na siku zitapita utajikuta siku ya kuja kuamua unaamua kuamuua kwa vile hakuna namna.

Tabia Ya Kulaumu. Kuna watu wanapebda sana lawama. Kika utakalofanya atalaumu. Atalaumu Serikali, atalaumu hajashirikishwa,atalaumu kuwa hajapewa nafasi, atalaumu hajapewa feedback. Watu wenye tabia ya kulaumu mara nyingi sana huwa hawajijui kuwa tabia ya kulaumu. Sababu ya watu kuepuka lawama mara nyingi sana watu wanaamua kukuepuka sababu wanajua una lawama katika mambo mengi kuliko mchango wa ustawi wa jambo. Lawama huwa hazina mchango katika maendeleo zaidi ya kubomoa.

Ingawa tabia ni suala la Mtazamo lakini mara nyingi sana wenye tabia zenye changamoto huwa wanaepukwa.

Monday, September 26, 2016

Tuesday, September 6, 2016

Bank Ya Maendeleo na Grace Products Waidhamini Gospel Star Search

Siku ya Jana Mradi wa GSS umeingia katika makubaliano na Bank Ya Maendeleo na Kampuni Ya Grace Products kwa ajili kufanikisha hatua ya Nusu Fainali na Fainali.

Makubaliano hayo yaliingiwa jana Katika Hotel Ya Regency na Kwa hatua hiyo Maendelo Bank na Grace Products wanafanyika kuwa Wadhamini Wa Shindano hilo la Gospel Star Search.

Mratibu wa Mradi huo Sam Sasali alieleza kuwa Ufadhili huo wa Kampuni hizo mbili utazidi kuleta chachu katika hatua ambayo mashindano hayo yamefikia.

Siku Ya Jana Wakati Wa Kuwekeana Saini katika Hotel ya Regency
Baadhi Ya Waandishi Siku Ya Jana
Mratibu wa GSS Sam Sasali akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari

Mwakilishi wa Maendeleo Bank Mr. Tarimo akiweka Saini katika Hafla hiyo huku Meneja wa Tawi la Luther House Ms. Margareth Msengi akiwa anashuhudia tukio hilo


Mkurugenzi wa Grace Product Bw. Siza akisaini Makubaliano mbele Ya Waandishi wa Habari.
Wadhamini wa GSS Wakiwa na Timu nzima ya GSS

Tuesday, May 24, 2016

Papaa On Tuesday…..Akugeukaye Hufunza Pasipo Jitambua

Umewahi sikia mtu anaitwa msaliti ama vijana wa kileo wanaita “Snitch”?Hakuna Msaliti ambaye aliwahi dhaniwa, na ikitokea kuwa alikuwa anajulikana tangu zamani maumivu yake hayafanani sana na yule ambaye hukumtarajia.

Hakuna Usaliti unaouma kama ule wa mtu ambaye ulimwamini mko wote siku zote. Nimewahi sikia wasaliti wa mapenzi, nimewahi sikia Wasaliti wa Ajira, nimewahi sikia Wasaliti wa Imani Fulani ila mara chache sana nimewahi sikia Watu waliosaliti nafsi zao wenyewe.

Wakati nikisoma Shahada ya Kwanza katika Chuo Kimoja hapa Nchini Mwalimu wangu wa Somo la “Human Behaviors” Mr. Fatty aliwahi sema “Tabia za Mwanadamu hazitabiriki, mtu anaweza kuja leo kwako anaomba kazi mpaka analia akasema hata iweje hata hama Ofisi yako ukamuamini, ajabu ni kwamba unashangaa baada ya Mwezi mmoja anaweza hama Ofisi yako…Human Behaviors are unpredictable”.


 Yuda pamoja na kukaa na Yesu siku zote akamsaliti, unaweza kuwa na mpenzi wako ukamsomesha hadi Chuo Kikuu, siku anayo graduate chuo ndo siku hiyo hiyo ana graduate na uhusiano wenu. Unabaki na maswali kuwa kweli umeachwa?Tabia ya Mwanadamu imefichwa ndani ya mazingira na wakati.


Kama ingekuwa unajua Fulani katika maisha kuna siku atakusaliti basi nina amini kabisa hakuna mtu angekuwa yuko tayari kuwekeza muda, fedha na hali kwa mtu ambaye siku moja atakuja kumuumiza nafsi yake.

Msaliti mara zote ameonekana kama mtu ambaye hafai na yamkini hata kuishi sio ruksa kwake. Ukweli ni kwamba kuna watu baada ya kusalitiwa ndipo siku hiyo walijitambua katika maisha yao.

Usaliti ulisababisha akili zao kufunguka, Msaliti alisababisha aitafute njia sahihi ya maisha baada ya kuwa amepotea njia. Leo hii kuna watu wanafurahi sana kwa kuwa miaka michache ama mingi iliyopita mwajiri wake alimsaliti katika makubaliano yao ya ajira.

Kuna watu baada ya kufukuzwa kazi ndipo walipopata kazi bora na njema kuliko ile waliyofukuzwa. Kuna watu baada ya kuachwa na Boyfriends na Girl Friends zao ndipo walipokutana na Wapenzi wao wa sasa ambao walikutana baada ya kuachwa, kuna watu ambao walikuwa wanafanya biashara na watu Fulani baada ya mafanikio ya Kibiashara waligeukwa kama sio walizungukwa wakajikuta katikakati ya madeni na hasara kubwa ajabu ni kwamba leo hii ni watu wenye mafanikio makubwa katika Biashara. Ukweli ni kwamba Usaliti ulifanyika ni Elimu bila ada ingawa ilikuwa imeambatana na maumivu.
Furaha ya Mtu aliyekusaliti ni Kuona hausimami tena, maumivu ya msaliti huwa makubwa pale inapotokea ukajipanga upya na kuanza kupiga hatua kuelekea katika mafanikio. Msaliti hukosa nguvu na hamu pale anapokutana na mtu aliyemsaliti halafu amekuwa na maendeleo kuliko wakati anakusaliti. Kuna wakati ni vema tukawashukuru wale waliotusaliti maishani maana kupitia wao kuna wengine waliongeza speed za maisha na kusaka hela ambazo leo hii umefanikiwa sababu ya “Catalyst” ya Usaliti.

Jambo Lolote ukiamua kulipa maana linakuwa na maana hata usaliti unaotokea kwenye maisha ukiamua kuupa maaana chanya nao utakuwa na maana kwako.

Tuesday, May 10, 2016

Papaa On Tuesday.....Ukijitambua Utaifahamu Thamani Yako.


Kati ya vitu ambavyo wanyonyaji wengi Katika soko la ajira wanavitumia kimojawapo ni kuzuia wafanyakazi wao kutambua “HAKI ZAO”. Ukishindwa kutambua haki zako Utashindwa kuwa na Ujasiri katika mambo mengi. Kwa miaka 7 ambayo nimekaa kwenye Soko la ajira kama Mwajiri niligundua kuwa hakuna “Management” inayompenda mtu anayejitambua. Mara nyingi sana “Menejimenti” zinaamini mtu anayejitambua anakuwa mkorofi na anaweza kusababisha wengine pia kujitambua na kuanza kudai “Haki” zao.

Tofauti na kwenye mapenzi na ndoa Mtu anayejitambua huku ndiye ana thamani kubwa. Kwa kadri Mwanaume anapojitambua Kimajukumu basi “Haki” yake kutoka kwa Mke wake sio suala la Maandamano. Ukiona Mume ama Mke anasotea sana “Haki” yake basi jua kuna Jukumu halijatekelezwa kikamilifu. Bado tupo kwenye Zama ambazo tendo la ndoa linaweza tumika kama kitu cha starehe ama kifaaa cha adhabu katika mahusiano.


Thamani ya mtu imefichwa katika kujitambua. Watu wengi hudhani Kujitambua maana yake ni Kuacha kuajiriwa na Kujiajiri SIO KWELI. Nimekutana na watu kibao ambao waliacha kazi kwa ajili tu kuhamasika na story story za watu walioacha kazi alipofika mtaani mambo yamekuwa tofauti huyu naye HAJITAMBUI. Wapo walioajiriwa nawafahamu wanaojitambua pia. Wapo wanaodhani kuwa na Shahada ya Kwanza ama Ya Pili ni Kujitambua, Si kweli nimewahi kukutana na Maprofesa ambao hawajitambui. Kujitambua ni Zaidi ya Kuongea Kiingereza, Kujitambua ni zaidi ya Kukariri Misemo ya watu wa zamani akina Aristotle, Carl Max, Jimmy Carter na wengine.

Mtu anayejitambua najua thamani yake, anajua nini anachokitaka maishani, anayejitambua anafahamu maamuzi anayoyachukua katika maisha na gharama ya maamuzi hayo, mtu anayejitambua hasukumwi na vishawishi, anayejitambua ana Ujasiri, anayejitambua anafahamu thamani ya Kujitambua. Wapo wengi sana ambao wamepelekwa kusoma na Kampuni ama Mashirika lakini ukweli ni kwamba Elimu badala ya Kuwakomboa ndio kwanza imewakomoa wamejikuta katika Kitanzi cha Utumwa uliotukuka.

Siku Ukijitambua utafahamu kwa Kiasi gani Watu wamefaidika kupitia wewe, Ukijitambua Utafahamu ni Kwa namna gani umekuwa ukinyonywa na anayekulipa, Siku Ukijitambua utagundua kwanini umepoteza wateja wengi katika Biashara, Siku Ukijitambua Utagundua aina hiyo ya Mwanaume ama Mwanamke unayemuwaza na Kusubiri kwa sasa ana miezi 3 tangu azaliwe.

Ukijitambua utajua thamani, Wajibu, Haki na Kule unakotakiwa kuwa kwa sasa.


Return Of The Giant.


0713494110

Friday, February 12, 2016

Njia Ipo Ukiitafuta

Good Morning.
Kwenye maisha kuna wakati utajikuta unalazimika kuanza upya baada ya kile ulichokuwa nacho kupotea ama ulichotarajia haujakipata.

Nimesoma habari za wengi na nimekutana na watu wengi sana ambao walifanikiwa kuanza upya na kutimiza malengo yao baada ya kupitia hali ngumu maishani mwao.Kuna mtu alipoteza familia yake yote Kwenye ajali akabaki peke yake akaona kama vile maisha yamefika mwisho lakini baada ya kuwa tayari kuanza upya na kukubaliana na yaliyotokea leo ameweza kuyashinda maumivu yote na amefanikiwa kufikia ndoto yake.

Baada ya kushindwa kuendelea na shule na kujikuta akiishi maisha ya mtaani baada ya wazazi wake kuachana akiwa na umri wa miaka 7 alikubali kuanza upya na leo Anthony Robins ana utajiri takribani dola za kimarekani 400m,anamiliki ndege, majumba makubwa etc .

Baada ya kupitia mateso na uchungu wa kubakwa akiwa na miaka 14  na kukataliwa mara nyingi alipoenda kutafuta Kazi za utangazaji,Leo Oprah Winfrey sio tu anatangaza bali anamiliki vyombo vya habari,ALIAMUA KUANZA UPYA.

Baada ya Steve Jobs kufukuzwa Kwenye kampuni ambayo aliianzisha yeye mwenyewe,hakukata tamaa ya kutimiza ndoto yako.ALIAMUA KUANZA UPYA.

Umefeli mtihani,umeachwa na umpendaye,biashara yako imefilisika,umepoteza kila ulichonacho,umefukuzwa kazi...Usikubali kukaa chini na kuanza kulia.AMUA KUANZA UPYA LEO.

Naona ndoto yako ikitimia, naona ukiwasaidia wengi kufanikiwa kutokana na historia yako,naona ukiinuka na kuwainua wengi watakaopitia hali kama uliyopitia.
Naamini Katika ndoto yako,
Naamini Katika Uwezo Wako,
Naamini Katika Hatima Yako.

By Joel Nanauka

See You At the Top.
Tembelea (www.JoelNanauka.Com)  Ujifunze Zaidi

Sio Kila Mtu wa Kubeba Katika Maisha

Kama Unasafiri unaenda Arusha huwezi Jichanganya na abiria wa Mbeya ukifika pale Stend ya Mabasi Ubungo kwa wakazi wa jiji la Dar. Kama unaenda Mtwara ama Lindi huwezi kwenda Ubungo utaenda Mbagala... Kama Unaenda Na Ndege ukifika Airport kuna abiria wa ndani na abiria wa nje, na kila abiria anaondoka na ndege yake na muda wake na kila mtu ana Seat yake na kila mtu ana namba ya Seat yake. Ukiwa unaenda Zanzibar hauendi  Stend ya mabasi Ubungo. Kila safari ina kituo chake,  ina watu wake na usafiri wake.

Unaweza shangaa unafika kituo chako cha safari ukashangaa kuna watu wengiii ukadhani umekosa tiketi kumbe wengi ni Wasindikizaji tu. Unaweza kuta mtu mmoja amesindikizwa na watu kumi. Sio kila mtu ni Msafiri wengine ni wasindikizaji.
Kwanini unakaa na watu ambao hamuendi safari moja ya maisha?kwanini unang'ang'ania kupanda na mabegi mazito ndani ya gari wakati kuna Buti za gari? Mwaka 2016 umeanza umeyabeba mambo mazito ya mwaka 2015, umebeba mizigo ya watu, mawazo ambayo inakulemea kupiga hatua za maisha. Kuna Mizigo hutakiwi kuibeba kuna watu hutakiwi kuwabeba unapaswa kukutana nao mwisho wa safari. Mzigo wa kwenye buti unapaswa kuuchukua mwisho wa safari.
Usikazane kuwa na marafiki wasiokwenda safari moja na wewe, usiwabebe watu ambao hamuendi safari moja na wewe ya maisha hata kama ni Mpenzi wako. Usibebe vitu vinavyopunguza speed ya kuelekea kilele cha mafanikio yako. Unajikuta muda mwingi unawaza vitu unawaza watu unawaza ulivyoumizwa unawaza ulivyopata hasara.

Hakikisha unasafiri na watu sahihi hakikisha unaenda kituo sahihi na Class sahihi. Ukitaka kupanda First Class lazima ulipe gharama.
Maamuzi yako yanayotegemea watu wenye akili mnazo fanana mtaamua mambo yale yale namna ile ile na matokeo yatakuwa yale yale. Jiongeze mwaka 2016 piga chini wasiokwenda na wewe.

Think Differently, Make a Difference.

Saturday, January 9, 2016

Heaven On Earth Season 5 Hakunaga

usiku wa leo katika Ukumbi wa CCT Mzumbe University imefanyika Event ya kusifu na Kuabudu yenye Jina la Heaven On Earth ikiwa safari hii ni msimu wake wa 5. Event hiyo yenye kujumuisha wanafunzi wa madhehebu mbalimbali pasipo kujali itikadi zao imefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kutoka Mkoa wa Morogoro na vingine Dar-es-Salaam vilishiriki Mkesha huo. Mbali na Wanafunzi hapo Pia walikuwepo wanamuziki wengine kama Angel Bernard wa Sakafu, Mzee Cosmas Chidumule, Lulu, na Nuru Choir kutoka Mzumbe.

Mkesha huo ambao ukifanyika kila mwaka katika chuo Kikuu Mzumbe umefanyika katika mafanikio makubwa, Crew nzima ya Kiango Media na Chomoza Ya Clouds Tv walikuwepo kufuatilia tukio moja baada ya Jingine. Habari Kamili fuatilia Chomoza ya Clouds Tv kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 4 asubuhi Kila siku ya Jumapili.

Kusikiliza Kiango Online radio download app kwenye play store yenye jina "Kiango Radio".

Mwenyekiti wa USCF akitoa zoezi la Utambulisho wa waliohudhuria tukio la leo.
Drummer Boy akiwa akienda sawa...
Angel Bernard Sakafu akiwa kikazi.
Angel


Lulu akiwa katika Jukwaaa usiku wa Leo
Kikundi Cha Fellowship ya Katoliki wakiwa ndani ya Heaven On Earth.


Mc namba 2 akiwa anaenda sawa
Mc namba 1kazi kazini..

Tuesday, December 22, 2015

Papaa On Tuesday.....Umaalum Sio Umaarufu.

Nadhani kati ya Watu ambao hawatajwi tajwi sana hata Makanisani kwenye Mafundisho ni Yusuf Baba yake na Yesu. Wakati Mwingine hata nyimbo wametungiwa akina Goliath lakini Yusuf Baba yake Yesu amesahaulika sana kuimbwa. Unadhani Yusufu hakuwa na Umuhimu wakati wa Maisha yake?Watu wengi tumejikuta tumetafuta sana Umaarufu na kutambulika kwa watu wakati hatuna mambo ya Msingi tunayofanya kwenye maisha yetu binafsi na Jamii kwa Ujumla wake. Katika maisha niliyoishi nimekuja kugundua watu wanaofanya mambo mengi sana ya kimaendeleo sio wale maarufu. Watu Wasio Maarufu wanawatumia Watu Maarufu kuendesha maisha yao.
Umuhimu wa mtu unapimwa katika “Role” anayoitumikia ama kama ni Movie basi katika “Scene” anayoicheza kama ni kwenye jamii majukumu anayoyatekeleza. Wakati huu wa Christmas ndio wakati pekee kwenye mafundisho tunamkumbuka Yusufu tena kwa Juu Juu. Lakini ukweli “scene” aliyoicheza Yusuf ni ngumu ambayo Wanaume wengi sana wa Kizazi chetu wasingeweza kuishi na majukumu hayo.

Yusuf alikuwa anafanya kazi inayodharaulika kwenye jamii yake ndo maana walikuwa wanamwita Yesu mtoto wa “fundi mbao”. Sio kazi ya watu ambao wanakipato sana. Mbaya zaidi akiwa katika mazingira hayo hayo akawa anampenda Mungu sana ndio maana anaitwa mtu wa haki. Katika hali zake hizo mbili ghafla mchumba wako ambaye umejichanga changa changa uweze kumuoa unakuja sikia Mjamzito. Unapoamua kumpiga chini ghafla Malaika anakutokea kuwa uukubali tu ule ujauzito na uulee. Hivi jamii itakuelewaje kuwa eti Mtoto ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu wakati hakuna hata siku duniani kuna Mwanadamu wa hivo amewahi tokea kupata mimba bila kudungunyuliwa. Hata kama utakubali lakini kipato chako sasa kinaruhusu Kumkuza huyo mtoto?Tena ingekuwa kizazi hiki anataka na Pampas, Daipaz, Maziwa ya Kopo n.k nadhani uamuzi wa Yusufu si tu sababu ya haki lakini pia ilikuwa inahitajika Moyo kukuza mtoto wa Mwanaume mwingine kama mwanadamu wa kawaida.

Unatakiwa utimize majukumu kama Mume na kama Baba katika jambo ambalo kimsingi umeaminiwa. Kutapikatapika kwa Mariam Yusufu yupo, Ghafla akiwa mjamzito Wasafiri kwa Punda, hapo ndo kasheshe siku hizi na Baiskeli tu issue je na Punda si balaa. Pa kujifungulia kwenyewe ni kwenye holi la kulishia wanyama, hivi ni nani alimsaidia Mariam Ku Push, ni nani alimsaidia Mariam kukata lile Kondo la Uzazi?Ni nani alimsafisha Mtoto, ni Nani alikuwa anahangaika na maziwa ya Mtoto wakati huo wote Yusufu anahangaika kumbuka Mtoto sio wa kwake kibaolojia kwa Umuhimu huu Kutokutajwa kwake haimaanishi kuwa hakuna Kitu alifanya. Yusufu alitakiwa tengeneza BOND na mtoto tangu akiwa mdogo, BIla Yusufu Yesu asingeenda Hekaluni akiwa na miaka 12.

Nimejaribu kukuonesha Umuhimu wa mtu pasipo Umaarufu wake. Delila aliyemrubuni Samsoni ni Maarufu Kuliko Yusufu. Tumejikuta tunatumia Muda mwingi sana kutafuta kuwa maarufu kwa namna moja ama nyingine na kusahau kusudi la wewe kuwepo. Afadhali Umuhimu wako ukupelekee kwenye umaarufu kuliko kudhani umaarufu utakupa Umuhimu kwenye jamii. Ni rahisi sana kuwa maarufu lakini kama huna Umuhimu kwenye Jamii utasahaulika kesho tu. Kuna watu kazi zao mambo yao yamekaa kizazi na kizazi wanajenga familia zao, wanajenga ndoa zao wanajenga taaluma zao pasipo kujulikana na yeyote. Wakati mwingine ni afadhali usijulikane kwa watu kwa maana ya umaarufu lakini ukawa na umuhimu mkubwa katika Jamii.

Usisumbuke kutengeneza jina kabla hujatengeneza umuhimu wako katika maisha yako. Watu wanasema nini juu yako, Je watu ambao wanakuongelea kwa umaarufu wako wanafaidika nini na kuwepo kwako katika Jamii. Nini kinatengeneza Umaarufu wako Nyimbo?Uandishi?Kuchekesha?Umewahi kuwaza kuwa itachukua muda gani tangu kufa kwako na kusahaulika kwako duniani?utakumbukwa kwa umaarufu ama umhimu wako katika wako?

+255 713 494 110

Friday, December 4, 2015

Recent Posts

Google+ Followers

Blog Archive