The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Saturday, July 24, 2010

Wednesday, July 21, 2010

Papaa On Tuesday....Mfumo Wetu wa Elimu Unatufanya Tuwe Watumwa Wa Maisha

Wakati kila kona ya nchi mchakato wa kuelekea uchaguzi wa majimbo unapelekea joto la homa ya uchaguzi kupanda, basi tuungane na kuwatia Moyo Marafiki Huru waliojitolea kwenda kugombea Ubunge, ukipata kanafasi basi mtumie sms ya kumtia moyo na kumpa matumaini katika Kristo Yesu.

Kuna kitabu cha Robert Kayosaki kinaitwa "If You want To Be Rich and Happy, Dont Go To School" na Kitabu Cha George S. Clason kinaitwa "The Richest Man In Babylon" kama huna hivi vitabu please vitafute. Jiulize unafanyia nini kipato unachokipata either kazini, Chuoni ama Kwenye Biashara. Last week nilikuwa na Presentations pale Ardhi University on Personal Financial Management basing on "Practicle Experiance". Sio theory ina semaje ila wapi nimeanguka wapi nime weza wapi bado pana ni challange na Biblia inasemaje kwenye hilo. Niwashukuru Ann, Milembe na Protace ambao walikuwa pamoja nami katika Siku zile pale Ardhi University.

Graduates wengi sana sasa ndo wametoma vyuoni wapo mtaani, nakutana nao wengi sana na kuwasiliana nao, kila unayekutana nae "Brother nitafutie Kazi", ukikutana na mtu hajasoma nae "Brother nitafutie Kazi" what is the difference kati aliyemaliza shahada ya kwanza na asiye maliza. Tuliwahi utazama mfumo wetu wa elimu mwisho wa siku wote unatufanya tuwe watumwa wa maisha yetu wenyewe.

Tangu enzi za akina Masauni wanasoma Mpaka sasa haiwezekani majibu ya essay ya History yakawa yale yale "Factors Of Abolition Of Slave Trade" kila siku teh teh teh yale yale "Humantarian Reason", hahahaha Scramble and Partition For Africa majibu yale yale, huu usomi gani hauna jipya, Tangu enzi zile kitabu maarufu cha hesabu shule ya Msingi "Hisabati Za Kikwetu", Secondary hesabu ni zile zile Standardazation and Exponants, najiuliza kwanini nisisome Mto Msimbazi ama Malagalasi, eti nasoma Zambezi na Mississipi, teh teh Swali la Geography "What are economical Activities That are taking Place at Lake Zambezi"? hahaha eti hizo hizo ndo pia kwenye Mto mwingine jamani huku si kukariri, hahhahah Economics tangu enzi za akina Ipyana Mzumbe Factors for Inflation ni zile zile?hahahah ni kweli Mwombeki issue za Internal Medicine ama Pathology hazibadiliki?Wakati nasoma Financial Management chini ya Mwalimu wangu Kibasa niliwahi soma issue za Profit ratio na njia zake za Pharmacetical sijui nini nini huko. Mwisho wa siku mie ninaitwa "Human Resource Manager" tutafute uhalisia, tunayoyasomea ni kwa asilimia ngapi ni yanafanana na yale tunayoyafanyia kazi?na Je ni kweli kabisa kabisa kazi unayoifanya ilikuwa inakupasa uwe na degree?kweli kabisa be honest, kama sivyo basi Mfumo wetu wa Elimu unatutayarisha kwa kitu nadhalia na sio halisia. Bora tusome tu zile "Assimilation Policy"

Jumamosi nilikwenda kufanya presentation kwa baadhi ya wajumbe Kampuni fulani ya mambo na Kahawa, pamoja na Wadau wanaonunua Pamba kwa wakulima wadogo wadogo na kuuza katika Soko la Dunia. Hiyo deal niliunganishiwa na Rafiki Huru hapa hapa, aliyenipa material ya presentation ni Rafiki Huru mwingine huwezi amini mwanaume nikajipinda kuongea na kushusha nondo, wakati narudi nikawa naenda Ardhi University, njiani nikawa najiuliza "hiki ninachikifanya nikiivest kwa muda wa mwaka mmoja" nitakuwa wapi?nikajiuliza ni-ivest kwenye hili ama nikasome Masters ya Human Resource Management?hahahahahha think Of it. Lazima ujijengee mfumo wa kiji evaluate na kufanya maamuzi magumu pia, jichunguze still niko njia sahihi ama si sahihi, unajua kuna watu wanawapenzi na kwakweli wanajua wamepotea lakini hawana jinsi?hahahah Course ya Chuo ulikosea, kazi unayofanya umechemsha, Mme ama mke nae uko chaka?khaa lini utakuwa wewe mwenyewe?Yakobo akasema "Lini Nitayaangalia Mambo yangu Mwenyewe"?

Hata wanaojiita wasomi wamenishangaza waalimu wangu kabisa yaani wanataka niwaunganishie deal za Consultations hapa mjini khaaa najiuliza kabisa, huyu mwalimu ana akili kweli?ninakaa nakuwaza, mtu kama Prosper amesoma Political Science and Public Admin hahaha yaani Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma hahahaha wala hayupo huko, A-Level kasoma Kifaransa Language na French (KLF) hahahah huyu Jamaa siku hizi ni Mjasiliamali na ujasiliamali unampa connections za Biashara kuliko PSPA hahahah huyu jamaa amepoteza miaka 5 kwenye kitu kinachoitwa elimu ya Juu, wengi tunasoma ili tupate kazi?wengi wanataka kusoma Masters ili walipwe mshahara Mkubwa, jiulize kweli kabisa kabisa unahitaji Masters ama PHD?na kama unahitaji lini?na yanini?. Akili za Layman hazijui what is called "Stages Of Decision Making" hazijui kabisa....Ok na sie tuliosoma "Decision Making" mbona hatufuati wakati wa kufanya Maamuzi?Mbona wengi tunafuata maamuzi ya waajiri wetu hata kama si ya kitaaluma?wengi tukitishiwa kufukuzwa kazi tunakuwa watumwa kwa wale wanaotuweka mjini, wadada wengi wananyanyaswa sehemu za kazi, watu wengi wanachukia kwenda kazini kuliko kwenda nyumbani, watu wengi wanaendesha magari huku wanamawazo, wengi ndoa bado vimeo.

Kaa sikumoja jiulize hali uliyonayo utaendelea nayo mpaka lini?na kama hujaridhika na maisha unayoishi unafanyaje kujikwamua?are you serious unataka kutoka?. Mfumo wa elimu wa mwalimu kutuandikia notes yaani amesoma kwa niaba yetu, unapelekea siku zote kwenye maisha kuwe kuna madhara kwa baadhi yetu. Mie nijitolee mfano. zamani nilikuwa napenda sana kuambiwa, yaani nauliza, hivi jamani viwanja na mashamba vinapatikana wapi?basi mtu ananiambia, then namwambia kaniulizie kama vipo, anasema haya, akisema vipo kisha nasema, siku ukiwa unaenda utaniambia?unajua madhara yake?kila kitu ukisubiri mtu afanye ndo wewe ufanye hautafanya, ukiongea na mtu kitu mbananishe kama yeye haendi mwambie akuelekeze, niliwahi jiuliza wenzangu wanaojua huwa wanajuaje?kwanini nisijifunze?wanavyofanya, kujifunza na kukosea ndo usomi wa kweli, kuna tofauti kubwa sana ya mtu nayefundisha Business Adminstration akiwa hana hata genge la nyanya na yule anayefundisha Business Adminstration huku ana genge la nyanya.

...//Papaa

Saturday, July 17, 2010

Sunday, July 11, 2010

Thursday, July 8, 2010

Papaa On TUesday.....Ukizimia Siku Ya Tabu Nguvu Zako Ni Chache

Ingawa nimekuwa nikiandika Papaa On Tuesday kila Jumanne, lakini kuna POT ambazo hata mimi mwenyewe huwa nina zi feel sana kwenye maisha yangu. Kila Moja inauzito wake lakini kuna Papaa On Tuesday ambazo nakumbuka niliziandika huku Machozi yakinitoka sababu ya memory zilizokuwa zikipita kichwani kwa kadri nilivyokuwa nikiandika na kuzisoma.

Kati ya POT hizo mojawapo ni hii ya Kuzimia Siku Ya Tabu. Unajua unaweza ukawa unajiona ngangari, unaweza kutatua matatizo ya watu, unaweza ukawa pouwa tu na ukaonekana stable kumbe bana hujakutana na jambo la kukutikisa. Ukipata jambo la kukutikisha ndio utajua how strong uko. Tatizo ama matatizo wakati mwingi sana hudhihirisha tabia zetu zingine zilizojificha. Inawezekana ukadhani mtu hana hasira kumbe hajapata fursa ya kukasirika, unaweza dhani mtu hana matusi kumbe hajapata mazingira ya kuropoka tusi, unaweza ukadhani Jamaa Mwaminifu kumbe hajapata mazingira ya Usaliti. Ukitaka kupima nguvu zako ni chache ama nyingi uwepo kwenye mazingira yaliyokuwa yana ku favor asilimia mia nane kisha ukachomoka salama. Ulikuwa na Uwezo Wote tena pasipo kutumia hata nguvu kidogo kutenda uovu lakini ukajiepusha nao.
Ni rahisi sana kuwanyoshea wengine vidole pasipo kujua sababu iliyopelekea mtu kuamua kile alicho kifanya. Nimewahi kukutana na watu wengi sana wanaojutia kile walichokifanya baada ya kukifanya sio kwamba walipenda kufanya. Mimi sina tatizo sana na kile walichokifanya ila nina tatizo na Uwezo wa Wao kutokurudia kufanya. Rafiki yangu Mussa aliwahi sema Watu wengi sana wanatumia nguvu kuzuia kuanguka kuliko kujipanga kimtazamo kuwa Nitasimamaje mara baada ya kuanguka katika Maisha. Kuna watu wameanguka kibiashara nba kushindwa kusimama tena, kuna watu wamewahi anguka kwenye mahusino. Kuna watu wamewahi kuanguka kimasomo, kila mtu ana namna yake ya kuanguka. Issue inakuwa what next baada ya issue kutokea. Unajipangaje upya baada ya KUHARIBU. Niliwahi andika Papaa On Tuesday Mwanzoni mwa mwaka huu kuwa ukiona Unajipanga Ujue Ulipanguka. Jipange Sawa Sawa Kuvunjika Kwa Koleo Sio Mwisho wa Uhunzi. Ukizimia Siku Ya Tabu Nguvu Zako Ni Chache.
Maisha yetu ya kila siku yamezungukwa na changamoto zisizo na Idadi, na mfumo wa maisha tuliyokulia wengi hayakutupa fursa ya kukabiliana namna ya kutafuta fumbuzi ya changamoto hizo. Tangu utotoni chochote kilichokuwa kinatukabili tunawaeleza wazazi, pensel ikipotea tunamwambia mama, wakati wa likizo tunaomba hela ya tuition, tukiwa shule swali likitushindwa swali la hesabu mwalimu atafanya kwa niaba yetu, kama kuna mwanafunzi machine kama Mozes Mwizarubi, basi tunampelekea yeye “atufanyie” Maswali na pengine tuna submit na kweli tunawekewa pata…matokeo yake mambo yote mepesi tuliokuwa tunafanya wenyewe yale yenye kutuhitaji tutumie akili zetu tuliwapa wengine,tukafaulu, tumeanza kazi na wengine tunafamilia, je kwa sasa yakija magumu tunapeleka wapi?hapa ndo kuna maturity ya mtu. Nakumbuka kila baba alipokuwa hana hela anasema subiri nirudi kutoka mjini, au njoo ofisini, nilikuwa najiuliza huko mjini kwenye hela ama Ofisini kwanini asije nazo nyumbani?Bwana we utu uzima dawa.

Papaa On Tuesday ya Leo inatoka katika Mithali 24:10. Ukizimia Siku Ya Taabu, Nguvu zako ni Chache. Sitaki ni fafanue kiundani, lakini tutazame neno nguvu ni kama uwezo, ability, capability,stahimili na uamuzi chanya baada ya tatizo.
Ukitaka kujua umekuwa kwa kiwango gani sio wakati kila kitu kimekaa sawa, Ukitaka kujua umekomaa kimaamuzi si wakati hakuna anayekusemea mabaya, ukitaka kujua ni kwa kiasi gani umekuwa si wakati mpenzi wako anakuchekea, ukitaka kujua umekomaa kimaamuzi sio wakati umepata promotion kazini maneno yanakutoka.

Unaongea nini unapopata Taarifa umefukuzwa kazi?unafanya nini pale yule uliyempenda kuliko kitu kingine anaposema its over, what do you do when a person you trusted ame-kucheat or lie to you.
Unaongea nini mtu uliyempa fedha zako akaamua kukuzima, mtu uliyekuwa unafanya nae biashara akikugeuka…..Ukiona umezimia kimaamuzi jua nguvu zako za kukabiliana na Changamoto za Maisha ni Chache na unahitaji nguvu kusimama.
Nikiwa Chuoni nakumbuka a woman I loved, a.k.a first lady ….Marafiki Zangu wanakumbuka unakuja jua unayempendaaaa ana-date na mtu mwingine, the same time Baba yangu ametolewa kwenye gazeti kwa Scandal na Jioni hiyo hiyo nilikuwa ninaanza Semina ya Siku tatu nakumbuka it was “Spiritual Emphasis Week” kwenye Fellowship. Nilikuwa nawakati mgumu sana sana mtu mzima nikaenda Valley (porini) nikaliaaaaaaa then nikaja chuo niko pouwa na kila mtu alikuwa anajua niko pouwa the only person ambaye alijua nakumbuka ni Mdada alikuwa anaitwa Lucy Kayombo hahaha wewe uliyezoea kuwatia watu moyo, kuwapa ushauri wengine yakikufika unajipangaje. .kuna wengine ukiwaambia watasema “Kha kama hata wewe limekupata hilo je sie?lazima tujifunze kutafuta fumbuzi za mambo na nguvu zetu kupimwa katika kila hatua ya tatizo tunayopitia.
Mambo yanapokuwa yanakukabili kwanza chekecha ubongo, tujifunze ku-sacrifice niliwahi wafundisha watu kuwa ukitaka kujua umekuwa ama lah kwaanza utaanza kuona una majukumu yanayokutaka wewe ufanye kama wewe, mfn. Kodi ya Nyumba, kulipia Karo za Wadogo zako,kulipa Luku, Kununua chakula na kununua mapazia na vyombo vya ndani na ku-Sacrifice kununua nguo mpya, blackberry na cheni ya gold basi jua umeanza kuwa mtu mzima kimaamuzi, ila ukiona unaachia kununua kitasa kipya cha mlango ulioharibika na unaenda kununua shati la kuvaa kwenye harusi wakati wewe mwenyewe umealikwa tena kwa kadi ya mtu mwingine basi jua level yako ya kuanza kukabiliana na changamoto za maisha bado iko Pentium one.
Changamoto pamoja na matatizo husababisha akili zetu zifanye kazi zaidi ya kawaida, Changamoto hupelekea ubunifu, Changamoto ina shape tabia zetu utajiuliza how?umewahi poteza nauli ukiwa Posta na unataka kwenda Tegeta?ile shida ina ku-provoke kufanya mambo ambayo si tabia yako utalala Posta?au wewe ni mdada unatoka Chang’ombe una drive ukiwa Buguruni tairi likapata Pancha tena uko peke yako unafanyaje? Na mtu uliyekuwa unadhani anaweza kukusaidia unampigia simu is not reachable kama ni u-Sister duu utakutoka ntakuambia, na akili yako itafanya kazi kwa kiwango cha tofauti sana . Au umewahi achwa na mtu uliyempenda sana kisha akakualika katika harusi yake, je utaenda?why utaenda, au hautaenda?na kama hautaenda why hautaenda?Ukizimia Tu siku ya Taabu nguvu zako ni chache. Au umewahi itwa kwenye Kikao cha Kanisa Mchungaji wenu uliyemuamini amepata Skando ya Uzinzi na Ubadhilifu wa fedha then wewe ndo upo unaulizwa toa mawazo unaongea nini?
Sisi ni Taifa la Sasa na Baadae wengine wameshaanza majukumu ya kifamilia na wengine bado,kama umezoea kila kitu kuongea na watu kuwahadithia watu basi jiandae kuaibika kama ni shida, kwa research yangu isiyo rasmi inaonesha watu wenye uwezo wa kutunza Siri wamepungua sana ukimwambia mtu saa hizi saa 8 anajua mwingine. Changamoto zije kutafuta msaada iwe ni njia mbadala baada ya kwako kushindikana. Tujifunze kukabiliana na Yale yanayotusibu kusumbuliwa na tatizo moja zaidi ya mara 5 hilo hilo kila mwezi hilo hilo kila wiki…basi wewe Jua unahitaji msaada zaidi.
Lazima tujiulize kwanini jambo fulani linatupata, kwanini kila nikijaribu kufanya Saving kila mwezi mwishowe unaila hiyo hela, kwanini kila mwezi lazima lazima nikope, kwanini kila relation ninayoingia inakuwa kimeo, kwanini ninapenda kuvaa nguo mpya, kwanini nikisoma kabla ya mtihani sielewi mpaka test itangazwe, kwanini naweza kuangalia tamthilia masaa 2 lakini siwezi kukaa lisaa limoja kuplan maisha yangu. Kwanini hata lile ninalo li plan na kulitafutia pesa hatimaye silifanyi?Je shida iko wapi?kwanini nikiambiwa Siri ya mtu yaaani lazima nitamwambia mwingine….Hivi kwanini wakati wa matatizo akili yangu haifanyi kazi?wakati mwingine hatujiulizi hivi kwanini mpaka sasa sijaoa?au kwanini mpaka sasa sijaolewa?ninatabia ya kujiuliza na kuandika, hivi kwanini hili linanisumbua na ninaandika ukweli sio hata mie mwenyewe najidanganya eti najipendelea……all its about me. Wewe keshao utakuwa na Kampuni yako, wewe Kesho utakuwa na Familia yao , wewe utawekwa katika sehemu ya kufanya maamuzi magumu either ya Kijamii au hata Kanisani kwenu utafanyaje? Wewe Jua Jambo moja Ukizimia Siku Ya Taabu Nguvu zako ni Chache.


Papaa Sebene
0713 494110

Tuesday, July 6, 2010

Saturday, July 3, 2010

Papaa On Tuesday.....Kwanini Ujipalie Makaa Wakati Uwezo Unao?

Leo Marafiki Huru nimekuja kivingine zaidi. Na leo sina Maneno Mengi sana . Sababu nina Uchungu.
Papaa On Tuesday inakusa kila Nyanja ya Maisha yetu ilituweze kupiga hatua katika maisha yetu.

Kila mtu anao wazazi, kama sio wazazi basi tuna walezi kama hatuna walezi basi tunao ndugu kama sio ndugu yeye ana familia. Kati ya changamoto iliyopo sasa hivi katika Kizazi chetu ni watu wanaoitwa “ndugu”. Zamani sie tuliokuwa tunaenda kulala kwa shangazi ama mama mdogo, au kwa mjomba, tuliokuwa Unapenda kwenda kwa Mama mdogo kwa kuwa wao walikuwa mambo safi zaidi. Si unajua za utotoni. Lakini siku hizi hawa ndugu dhu tunaunga unga sana , yaani sijui watoto wa mjomba waje kwako ama sijui umeenda kula na mpwa wako mmh imepungua sana . Ila bado kila mtu anao watu wa kuwaangalia kwa karibu.
Nilichotaka kuandika On Papaa On Tuesday nimeona nikiandike wiki ijayo niliongee hili kwanza. Inakusaidia nini wewe kuishi maisha ya ufahari na anasa wakati wazazi wako ama walezi walio kulea wanaishi kwa shida either kijijini ama hapa mjini. Mbona tunakosa shukrani kwa wale waliotulea?? Jana mchana nilipokea simu kutoka kwa mmoja wa wazazi wa marafiki zangu ambaye tumefahamiana tangu utoto ni kama tumekuwa pamoja. Huyu mkaka yupo hapa hapa dar na wazazi wake kwa sasa hawapo Dar, baada ya mzee wa o kustaafu. Mama wa huyu Rafiki yangu nimezoea kumuita Mama Mkubwa kwa kuwa aliwahi soma na Mama Chuo Cha Uuguzi huko Peramiho Songea. Mama Mkubwa Jana alinipigia akiwa kama analalamika mambo kama matatu.
1. Rafiki Yangu hawasaidii ndugu zake hata wale wa tumbo moja, yeye kama kaka mkubwa waliwahi muomba asaidiwe kusomesha wadogo zake kama wawili hivi lakini imekuwa utata, mara zote mpaka akumbushwe kumbushwe.
2. Dogo amekuwa haendi kuwasabahi wazazi kule waliko, yeye kazi kupiga simu tu kujua wanaendeleaje, tangu mwaka 2009 April alienda akakaa siku moja hajaenda mpaka leo. Kama kaka wa Familia wanatamani sana wakae kwa ajili ya maendeleo ya familia yao lakini kijana yuko busy
3. Kijana ana invest sana na mchumba wake na kuishi maisha ghali sana wakati wao kama wazazi hata zawadi hawajawai pata just ile willingly from him.

Niliumia sana sana kwa hili. Kwa kuwa dogo ninamfahamu sana.
Wazazi wetu ama ndugu zetu walijinyima ili sisi tuweze kuwa hivi tulivyo. Tunatoka familia tofauti tofauti. Biblia inasema “Waheshimu Baba yako na Mama yako ili uwe na Miaka mingi duniani?” mbona tunataka kufa kabla ya siku zetu???wengine ili tusome wazazi waliacha kujenga, waliacha kula vizuri, waliacha kuvaa vizuri
Inawezekana wazazi wako hawajasoma kama wewe uliposoma, wazazi wako hawana fedha kama wewe. Kabla haujaenda kula bata mlimani City jiulize je wazazi wako wakikukuta pale unakula na kuishi kwa anasa huku wamekuambia suala la mdogo wako kulipa ada watajisikiaje? Wadada nyie ndo wajenzi wa familia leo unakubali mchumba ama mume wako aitose familia yake kwa sababu yako basi dhambi ile ile itaturudia.
Wazazi hawataki tu hela, ndugu zetu hawataki tu hela they need us pia kukaa nao tu, kwa wale wazazi walio mbali wakati wa likizo nenda kijijini kaa kule hata wiki nzima fanya kazi kata majani ya ng’ombe kama mnayo, sahau u-boss wako wa huku dar. Kupiga simu tu haitoshi they need you than your calls. Wazazi wakifurahi wanafungulia Baraka toka mbinguni juu, wakinung’unika hizi hela zinazokupa jeuri zitapukutika. Hata kama wazazi wetu wamepitwa na wakati na sie tunaenda na wakati basi fanya kitu kwa ajili yao . Hata kama hawana shida ya fedha usisubiri kuombwa kama una mke pangeni utaratibu msiende kutembea kama wageni nendeni kama watoto wa familia. Kwa sie tulio mjini siku moja chukua wazazi wako nenda nao popote for a dinner, kwetu tunaitaga kupima afya…nenda kapime afya popote ambapo utaona umetumia..mbona tunaweza kwenda na akina Carol, White Sands, mbona tunaweza Ku-support Marafiki Huru, Mbona tunaweza kwenda kumfata Keziah Zanzibar Just to visit her with ur own money na haikuumi,eti kwa wazazi wako unasema umetoa sana….guys tusiache neno baya likatoka kwenye vinywa vya hawa watu kisa etu hatuwatazami. Kuna siku tutafanya “Marafiki Huru Parents day” inawezekana mzazi wako anaumwa kumbe Mwombeki anaweza msaidia, inawezekana Mzazi wako amedhurumiwa kumbe Nelly anaweza kumsaidia hiyo kesi, inawezekana Mama yake Andrew ana madeal pale Wizarani Marafiki Huru tukapata nafasi, Wazazi wetu watafurahi wakaona Watoto Wao wakiwa na Marafiki Zao Wameamua Kufanya Kitu wa Wazazi wao…Let Our Parents Be Proud Of Us.
Nimalize kwa kusema wewe kuishi kwa anasa wakati wazazi wako wanateseka na uwezo wa kusaidia unao tunatafuta laana. Dhambi ile ile tunayoipanda itatutafuna wakati huo umri wetu utakapokuwa upo kwenye Omega.//Papaa

Recent Posts

Google+ Followers

Blog Archive