The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Monday, March 7, 2011

Matumizi Ya Dawa Za Mitishamba (Tiba Asilia) Ni Sawa Kwa Wakristo?

Tiba ambazo zilikuwa zikitumika wa babu zetu kabla ya wazungu kuja na hospitals ilikuwa ni mizizi na baadhi ya majani. Kwa wale waliokuwa na maradhi Fulani basi katika Jamii moja walikuwa wakitumia miti au mizizi Fulani inayotumika kwa ajili ya tiba na walikuwa wakipona. Baada ya ya ujio wa Wakoloni hapa Tanzania hizi tiba zikabadilishwa na kuitwa tiba za asili. Watanzania wengi mpaka sasa hasa sisi wapendwa tunatumia “maombi” na “tiba zisizo asilia” yaani hospitali.

Wapendwa wengi kama sio wote tumekatazwa kutumia hizi tiba asilia sababu wengi tunaamini kuwa zina uhusiano na “roho chafu” na ninaamini hii si ule ukoloni mambo leo wa kuamini kila kitu kizuri ni cha kizungu, maana utasikia watu wanacheka kizungu, wanakunja nne kama wazungu, tuna ibada za kiingereza, tunaimba nyimbo za kizungu, tunakula kuku wa kizungu mbaya zaidi tunavaa nguo za wazungu a.k.a mitumba na sasa tumeikubali hii tiba ya kizungu na kuitupilia mbali tiba asilia.
 
Jana nilikutana na Mshirika Mmoja wa Kanisa moja lililo maeneo ya Mabibo mwisho ambao wao Kanisa lao hawaamini katika Tiba za kizungu wanamini katika majani na mizizi na wana shuhuda nzuri tu katika hili. Niliwahi msikia pia mchungaji mmoja akiongea katika Praise Power kuhusu utumiaji wa majani, matunda na mizizi katika tiba asilia.
 
Mchungaji wa kule Loliondo kwa kutumia dawa asilia aliyombiwa na Mungu mwaka 1996 na miaka ya 2000 imesababisha watu wengi kukimbilia katika tiba asilia na kuachana na dawa hizi za wazungu na hata “imani” yao ya kupona kupitia maombi. Kuna mpendwa nina mjua kabisa aliombewa baada ya kupata tatizo la nguvu za kiume, baadae huyu jamaa akanunua dawa za wamasai na akapona katika maelezo yake anasema “alishuhudiwa rohoni” kutumia hizo dawa asilia.
 
Tangu jana baada ya kuonana na hawa waumini wa kanisa la Tiba asilia nimekuwa na mawazo sana maana nakumbuka niliwahi pewa dawa ya kichina ya kupunguza kitambi ambayo ni majani ambayo nilitakiwa kuyachemsha na kisha kunywa kama chai. Na wengi pia tumekuwa tukitumia “Tiba Asilia” za wachina na wazungu na kuacha hizi za kwetu. Je kuna tatizo lolote kwa Mkristo kufunga safari hadi Loliondo na kupata Kikombe kimoja na kupata “uponyaji” wa maradhi yao. Kama si Loliondo basi hata tiba asilia za wamasai au za asili zetu kule vijijini.
 
Ninaomba ushauri kabla sijaanza dozi ya tiba asilia. 

 
…//Papaa 
0713 494110
Post a Comment

Recent Posts

Google+ Followers

Blog Archive