The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Monday, April 18, 2011

Harris Kapiga (HK 1) Awekwa wakfu kuwa Mchungaji Jijini Dar-es-Salaam

Nilifahamiana na Haris Kapiga mwanzoni mwa miaka ya 1990 enzi hizo tukiwa Amana Vijana Centre, Nimefanya kazi na Haris Kapiga katika katika Redio ya Praise Power, Pia tupo wote katika Kampuni ya Tanzania Gospel Music Promoters ni yeye aliyeni comment niingie katika Kamati Ya Maandalizi ya Tanzania Gospel Music Awards.

Katika Exclusive Interview ya Papaa na Harris Pale Mbalamwezi Mitaa ya Kawe, Harris alieleza kuwa anaamini umefika sasa wakati wa Yeye kusema ndio katika utumishi kwa maana ya uchungaji, katika maongezi yetu alinialeza wazi kuwa muda mwingi anatumia kuomba na kutafuta mapenzi ya Mungu katika wito huu ndio sababu vipindi vyake pia Clouds FM vipo Jumamosi na Jumapili asubuhi kabla ya saa za Ibada.
                                            Pastor HK 1 (Haris Kapiga)


Haris Kapiga aliwekewa mikono ya Uchungaji wa kanisa na Askofu David Mwasota tarehe 10 April 2011, chini ya huduma ya Naioth Gosepl Assembly.

 Mchungaji Haris Kapiga kwa sasa ni 

mchungaji wa Kanisa la Promised Land lililoko Sinza Kamanyola jijini Dar es salam.

 HK 1 kushoto (Haris Kapiga) akiwa na HK 2 (Hudson Kamoga)

 

Hongera Pastor!

 


Post a Comment

Recent Posts

Google+ Followers

Blog Archive