The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Friday, October 7, 2011

Kumbukumbu Haiozi....Yesu Kwetu Ni Rafiki
"YESU KWETU NI RAFIKI 
[WHAT A FRIEND WE HAVE IN JESUS] 
TENZI NO. 9, N.S [NYIMBO STANDARD] NO. 239".
By..JOSEPH M. SCRIVEN


Joseph M. Scriven ni M-Irish aliyeishi kati ya miaka 1819-1896, akiwa na umri upatao miaka 25 hv, aliingia ktk upendo na kuazimia kutaka kuingia ktk maisha ya ndoa. Siku moja tu kabla ya ndoa yao na mchumba wake, mchumba wake huyo alipoteza maisha ktk ajali mbaya ya kuzama majini mtoni baada ya kurushwa na farasi aliyempanda km sehemu ya maandalizi ya ndoa ambayo ingekuwa kesho yake.

Akiwa amekufa moyo, Joseph alisafiri majini toka kwao kwenda kuanza maisha mapya Canada. Akiwa Canada akifanya kazi kama Mwalimu, aliingia ktk upendo wenye nia ile ile ya ndoa na safari hii alimpata binti mwanamwali aitwaye Eliza Roche [siyo Rocha RH] ambaye alikuwa ndugu wa mmoja wa wanafunzi wake. KWA MARA NYINGINE TENA, matumaini na ndoto za Joseph vikatoweka baada ya Eliza kuugua ghafla Pneumonia [nimon ia] na kufariki dunia siku moja tu kabla ya ndoa yao madhabahuni [historia ikajirudia].

Pamoja na mapito yote haya IMANI YAKE KWA MUNGU ilifanyika msaada mkubwa sana kwake. Mapema baada ya kufariki kwa Eliza, Joseph alijiunga na Plymouth Brethren na akaanza kuhubiri Injili ktk kanisa la Baptist. Hakupata kuoa tena, lkn akatumia muda wa maisha yake yaliyosalia akijitoa mali zake e.g. mavazi, pesa na muda wake akiwasaidia/akiwapa wahitaji na akisambaza upendo wa YESU kokote alipokwenda.

Yapata majira yale yale ya kifo cha Eliza, Joseph alipata ujumbe toka Ireland kuwa mama yake mpenzi aliugua. Hakuweza kwenda kukaa naye akimuuguza, ila aliandika barua ya kumliwaza na kumtakia uponyaji ambamo ndan i ya bahasha ile aliweka moja ya mashairi aliyotunga yenye kichwa What a Friend We Have in Jesus [YESU KWETU NI RAFIKI]

 
Baada ya mauti ya Joseph Scriven, wakazi wa Port Hope, Ontario, Canada, ambapo alijitoa kwa sana ktk maisha yake, walijenga mnara wa kumbukumbu ya maisha yake [ukienda pale leo utaukuta na unaruhusiwa kuhiji]. Fikiria maisha ya huzuni na vizuizi/vikwazo kiasi hiki yamewavuta wengi kwa YESU kipindi hicho na hata leo kwa kupitia tungo zake zenye mguso Rohoni.
 By Douglas Majwala wa Marafiki Huru Forum
Post a Comment

Popular Posts

Blogger templates

Categories

Blog Archive

Google+ Followers

Subscribe Here

Popular Posts