The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Friday, September 7, 2012

Wafahamu Watumishi Wa Mungu 25 Maarufu Tanzania

Mungu ameibariki Tanzania Kwa Kila aina ya Baraka za Mwilini na rohoni. Leo na wiki chache zijazo nitakujuza Watumishi 25 ambao ukiwataja kwenye mikoa zaidi ya Kumi hapa Tanzania yamikini wameshasikika na unaweza pata comments toka kwa waumini wao. Kuna Makanisa ambayo pengine yamesikika zaidi kuliko kuliko majina ya watumishi hao ama kuna watumishi wamesikika zaidi kuliko hata Makanisa wanayochunga.

Kuna Watumishi ambao wamekuwa maarufu sababu ya huduma zao kwa Ujumla, Sababu utajiri wao, sababu za huduma zao kwa wanafunzi ama kwa program zao za mahali pamoja.

lengo la Makala haya si kutafuta nani yuko Juu zaidi ya mwingine ila kutoa taarifa kwa umma na kuwatia moyo watumishi hawa kuwa kazi yao imevuka mipaka ya mikoa na nchi.

Tahadhari
Yawezekana vigezo vyako sio vugezo vyangu katika kuwasilisha.

Apostle Maboya(Ni kati ya watumishi waliokuwa wakijitambuisha kama mtume miaka ya mwanzo kabisa ya 90,kipindi hicho ukisikia mtu anajiita mtume ilikuwa si jambo la kawaida kama ilivyo siku hizi)
Pia ni mwanzilishi wa kanisa la Revival Assemblies of God Tanzania

Mama Getrude Rwakatare, Ni mmoja kati ya wachungaji wachache Tanzania wenye uwezo mkubwa kifedha, pia ni kati ya watanzania matajiri wakubwa.Anamiliki Shule za St. Marry's International.
Ni mwanzilishi wa Huduma/Kanisa la Mikocheni "B" Assemblissies of God.
Ni Mchungaji mwanamke mwenye mafanikio zaidi hapa nchini


Mwalimu Christopher Mwakasege.Ni mmoja kati ya waalimu wa injili maarufu hapa nchini ambaye huduma yake ya uwalimu inakusanya watu wengi sana katika mikutano na makongomani anayofanya sehemu mbalimbali hapa nchini.Anaongoza Huduma ya New Life Crusade/ New Life in Christ.Mchungaji Christopher Mtikila.Ni Mchungaji wa kanisa ambalo wengi hatulijui jina lake.Ila ni mmoja kati ya wachungaji maarufu sana hapa nchini kwa miaka mingi hasa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 90.Ni mwenyekiti wa chama cha siasa cha upinzani hapa Tanzania na ni mpigania haki mashuhuri sana kwa miaka mingi.Ameshakamatwa mara nyingi sana na kushikiliwa na hata kufungwa.Amewahi pia kuishinda serikali mahakani mara kadhaa na amejizolea umaarufu sana kwa uwezo wake wa kuongea bila uwoga.Pia ni muhubiri na mwalimu wa miaka mingi wa Injili.Ibada zake za kwenye TV za miujiza kwa miaka mingi zinawavutia wengi.
Mtume Veron Fernandez wa Agape Ministry.Ni mmoja kati ya watumishi wa kwanza kabisa kuhubiri katika Television na kumiliki kituo cha television hapa Tanzania.Anamiliki kituo cha ATN kituo cha kwanza cha kikristo hapa Tanzania.
amejipatia umaarufu mkubwa sana kwa mahubiri yake ndani na nje ya nchi.


Askofu Moses Kulola wa Evangelist Assemblies of God Tanzania.Ni mmoja kati ya watumishi waliotumika muda mrefu zaidi pengine kuliko wengi tunaowaona siku za leo.Ametumika kwa karibu miaka 60 akihubiri injili kutoka vijijini hadi mijini hapa nchini na nje ya nchi.Aina ya injili yake na style ya mahubiri yenye kupenya ndani ya nafsi imekuwa ikiwagusa sana watu wengi.Ni muhubiri pengine mwenye watoto wengi wengi wa kiroho kuliko yeyote aliyewahi kutokea tanzania.Kanisa lake limesambaa karibu kila kona ya Tanzania

Nabii GeorDavie wa GeorDavie Ministry iliyoko Arusha ni mmoja ya watumishi wanaokuja kwa kasi sana hapa nchini hususani mjini Arusha.

Huduma yake ya uponyaji na miujiza imekuwa ikipata umaarufu mkubwa sana hapa nchini.


Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Mission na Huduma ya Hakuna lisilowezekana.
Ni Mtumishi wa kwanza kumiliki kituo cha Radio cha kiroho hapa tanzania (WAPO Radio FM) na gazeti la kwanza la kipentekoste (Msemakweli).
Amejizolea umaarufu mkubwa kwa ibada zake za maombezi anazoziendesha na huduma ya hakuna lisolozekana.Pia ni mwenyekiti wa baraza la makanisa ya kipentekoste Tanzania (PCT).
Amejizolea umaarufu serikalini hadi kuteuliwa kwenye tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi.

Blog Itaendelea Kukujuza Zaidi Kila Ijumaa

Post a Comment

Recent Posts

Google+ Followers

Blog Archive