The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Tuesday, March 26, 2013

Papaa On Tuesday....Kuna Malipo Ya Kila Season Unavyoitumia Duniani

Ninawasalimu Kupitia Jina la Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai. Ikiwa leo ni Jumanne ya mwisho ya Kwaresma na tukiwa tayari kwa ajili ya Kusheherekea Sikukuu Ya Pasaka ipo haja ya Kukutakia Pasaka Njema. Wengine wanafurahia ni muda wa kuungana tena na familia zao lakini pia wengine ni wakati wa majuto maana mshahara ulishaisha tarehe 15 na Wabongo sie Sikukuu bila Kura bado hatujasheherekea yote kwa yote Mungu bado ni mwema.
Papaa On Tuesday ya leo inatoka kwenye Biblia Kitabu Kile Cha Muhubiri Sura ile ya 3 ambapo kwa ufupi inaeleza Kila Jambo lina majira yake na Kusudi hapa chini ya Jua, there is a time for every season. Haya ni kati ya maajabu ya Mungu kwa wanadamu, kuna wakati wa kucheka na kuna wakati wa kulia, kuna wakati wa kufurahi kuna wakati wa kunyamaza, kuna wakati wa kuruka na kuna wakati wa kutua nothing last forever. Hakuna kinachodumu milele. Ndio maana Mvua hainyeshi Januari mpaka januari, Jua haliwako December mpaka December, kwa majira yalivyoamriwa automatically majira hupishana. Kila Kitu ni Season huwezi kulia siku zote kuna siku utcaheka tu tatizo ni kujua uko kwenye season gani, na unatumiaje season hiyo.
Leo Ninataka niongee Season nzuri sitaki kuongea habari za season mbaya tumeshasikia sana kuhusu habari mbaya lakini ipo haja ya kusikia habari njema. Kwenye Kukua kwangu tangu mdogo kuna majira Mungu alishaamuru yaje kwenye maisha yangu, sikuwa na jitihada za kutaka kuota ndevu, sikuwa na jitihada za sauti kubadilika wakati wa kubalehe, kwa wanawake hawakuwa na jitihada ya mabadiliko ya maumbile katika miili yao sababu season ilikuwa imeshawadia kwenye maisha yao. Yalipofika majira ya kwenda shule tulikwenda shule wengine leo wanalipa kwa namna walivyotumia majira hayo sababu season imekwisha na unatakiwa kuvuna kutokana na kile ulichopanda.
Watu wengi sana hudhani watadumu kwenye season maisha yao yote, kuna wadada ambao enzi zao aisee walikuwa gumzo, waliringa walidengua waka wasanifu wenzao na kuona wao ndio wao, waliitwa majina yote Cleopatra, sijui A Missed Angel In Heaven, kila jina walikuwa nalo wao, wakasahau kuna siku season itaisha watabaki kuwa Bibi Angel, Kuna wanaume ambao kuna majira walikuwa na hela za kufufuka mtu, walihonga walivyotaka walibadilisha bar kama wanavyotaka walifanya kila kitu na kusahau kuwa ile ni season na kuna malipo ya kila season, kile unachokipanda lazima ukivune katika majira ya kuvuna. Kuna watu ambao walipofika majira ya kwenda shule wao waliendekeza Ushalubaro, shule kwao haikuwa ya msingi pengine ni kutoka na uwezo waliokuwa nao familia yao walibadilisha kila aina ya viatu wanavyotaka lakini wakasahau yale ni majira yao. Kuna watu ambao nimewahi waona wakiwa vijana wanamtumikia Mungu leo ameitwa kule kesho kaitwa huku wakawa talk of the City, wakasahau ni Season yao na Kuna Kusudi kwa Kila Season. Majira Yakiisha Ujue na Kusudi limeisha kwenye maisha yetu. Huwezi kubakia Juu siku zote kuna watu watakuja nyuma yako, maana kabla ya wewe pia walikuwepo wengine ila wewe ukaja tofauti, na pia wewe jua kuna watu watakuja tofauti. Kwa wale wa Zamani wanaume wanaopenda Mpira enzi za Kizazi chetu alikuwepo Mtu anaitwa Juma Mgunda ambaye kwa ajili ya shoot aliwahi pasua mpira katika uwanja wa Mkwakani, Kulikuwa kuna Mtua anaitwa Hussein Masha, Kuna Mtu anaitwa Abeid Mzima, Kuna akina Zamoyoni Mogella, Juma Pondamali wako wapi hawa watu??Season imekwisha wamesahaulika, kwenye uimbaji walikuwe Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga, Walikuwepo Washirika Njatanjata chini King Kidevu Salvadoo, Walikuwepo akina Mzungu Four, walikuwepo akina Mwasumbi Wako wapi ni juzi tu hapo wamepewa Tuzo eti Waimbaji Wakongwe, huwezi kubaki vile vile kama ulivyo kila siku Jua jambo mboja huwezi kubaki hivyo ulivyo siku zote inategemea sana unatumiaje season uliyokuwa nayo.
Kila Season ina kizazi chake, unatumiaje kizazi ulichonacho na muda ulionao, leo hii nikisema Nirudi Chuo Cha Mzumbe ambako nilisoma shahadaya yangu ya kwanza, nani ananijua?utakuwa idadi ya wanaokujua inapungua kutokana na Kizazi kilichopo, Kizazi kinachokuja kama hakikujua umaarufu unapungua, kuhitajika kwako kunapungua, kuna kazi kubwa sana kubaki kwenye vizazi vitatu bado mchango wako unatambulika. Watoto wetu tukiwaambia habari za Mashujaa watanzania kama akina Kinjeketile Ngwale na Chief Mangungo watoto wanaona ni kama vile wale watu walikuwa ni wapumbavu sana hawakuwa na akili lakini kwenye season yao wale jamaa walikuwa ni Mashujaa, Kuna malipo ya kila season tunavyoitumia.
Huwa nawaangalia sihangaiki sana na mtu ambaye yuko kwenye season maana kweli ukimuhitaji hata bei yake naye imekaa ki-season, nani leo hamjui Rose Muhando, leo nani hamjui Christina Shusho kwani kabla yao kulikuwa hakuna waimbaji wa nyimbo za Injili, kila jambo ni season na season ina kizazi chake, Kizazi Kikipita ujue season inaelekea ukingoni. Leo mie ze blogger niko kwenye season, nitasafiri huku na kule watu watakupigia simu na kukupongeza na kukulaumu na kuomba ushauri wa mambo tofauti, nisibweteke asilani kuona hakuna kama mimi, ni kujua niko kwenye season na ninapaswa kuitumia season hii kwa kupanda mbegu njema.
Wengi wakiwa kwenye season zao hupata tabia za maringo, kujiona wao ni bora kuliko wengine, yamkini wewe ni boss ahapo ulipo basi unataka watu wajue wewe upo, wahenga walisema Cheo ni dhamana maana kabla ya wewe kuwa na hiyo nafasi kuna mtu aliwahi kuwa nayo kabla its a matter of season. Leo unadharau wanaume kwa kuwa unajiona wewe ndio uko kwenye market unawapanga wanaume na wanawake vile unavyotaka just put in your mind its a matter of time hakika utavuna kile unachopanda katika majira haya. Kuna wengi wetu tumejuta baada ya majira fulani kupita kwenye maisha yetu tunabaki kusema enzi zetu sisi, ukishasikia enzi zetu sisi......ujue season ilishaisha imebaki kuwa enzi. Marafiki zangu wale maarufu tusijione sisi ni bora kuliko wengine tujuae jambo moja kila jambo lina majira yake na Kuna Kusudi katika kila majira.

Leo yamkini unaitwa huku na kule, kuna vikao vikubwa vikubwa unaitwa, au pengine unapata tender nyingi, au pengine watu wanakugombania, au ukifanya jambo linakuwa na ushawishi na muitikio, ama umekuwa ukitafutwa sana kufanya jambo fulani basi usidhani Utabaki kuwa hivyo siku zote Kila Jambo lina Majira yake kwenye maisha, huwezi kubaki kuwa Mrembo ama handsome Milele, siku za Kutumia muda mrefu kwenye Kioo nazo zinaukomo, siku za Kutumia fedha utakavyo zina ukomo sababu Aliyekupa wewe ndiye kawanyima wao, ukitumia vibaya season yako malipo ni hapa hapa duniani sababu seasons zinapishana, huweza suffer milele, huwezi lia milele, huwezi pitia unalopitia milele its a matter of time mwaka jana na mwaka huu mwanzoni niliwahi andika Papaa On Tuesday...Everyone Has a Story.....gonga hapa kama hukusoma...http://samsasali.blogspot.com/2013/01/papaa-on-tuesdayeveryone-has-storyits.html

Think Differently and Make a Difference.

Ze Blogger
0713 494110
Facebook: Samuel Sasali
Twitter Sam Sasali
Skype: Sasali Jr.
Instagram; Sam Sasali 
Post a Comment

Recent Posts

Google+ Followers

Categories

Blog Archive