The Extent You Know The Truth, The Extent You will Enjoy Salvation

Thursday, August 29, 2013

Kuna Nguvu Katika Kusifu Na Kuabudu...By Dr. Huruma Nkone

Semina Kubwa ilifofanyika Katika kanisa la Bethel Christian Centre la Kijenge Arusha chini ya Pastor Sosi na kuendeshwa na Dr. Huruma Nkone wa VCCT kuhusu Kusifu na Kuabudu ilikuwa na mafanikio Makubwa.

Semina hiyo iliyokusanya maelfu ya washirika wa Kanisa hilo ilikuwa ya namna yake kwa sababu ya nguvu ya neno iliyokuwa ikitolewa na Mtumishi wa Mungu Dr. Huruma Nkone alipokuwa akihudumu Kanisani hapo.

Semina hiyo iliyokuwa maalum kwa ajili ya kusifu na kuabudu imekuwa na mafanikio makubwa. Dr. Nkone akifundisha katika Semina hiyo alinukuliwa akisema "Kuna Nguvu ya Mungu inayodhihirishwa katika Kusifu na Kuabudu katika ustadi, Viwango"

Siku ya Mwisho siku ya Jumapili jioni ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kuhudumiwa na Roho Mtakatifu kupitia Kusifi na Kuabudu. Kutokana na huduma hiyo baadhi ya marafiki wa blog wamedokeza na kusema ipo haja ya Pastor Nkone kufundisha nje ya VCCT kwa sababu ana mafuta ya tofauti pia wakidokeza pia "Nabii hana heshima nyumbani Kwake".
 Pastor Nkone akiwa na Mchungaji Mwenyeji Pastor Sosi.

Kwaya Ya Watoto

New Life Band

Post a Comment

Recent Posts

Google+ Followers

Blog Archive